19 Machi 2011 - 20:30

Russia imejiunga na China kupinga wazo lolote la kuweka vikwazo vipya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa duru nyingine ya vikwazo haitakuwa na natija yoyote ghairi ya kuharibu zaidi hali ya mambo.

Russia imejiunga na China kupinga wazo lolote la kuweka vikwazo vipya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa duru nyingine ya vikwazo haitakuwa na natija yoyote ghairi ya kuharibu zaidi hali ya mambo.Taarifa ya pamoja ya wanadiplomasia wa China na Russia imesema kuwa vigezo vinavyotumiwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kama vile ripoti ya hivi karibuni ya IAEA ili kuandaa rasimu ya vikwazo vipya dhidi ya Iran havina mashiko. Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imeitaja ripoti hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Yukio Amano kuwa imejaa uongo na propaganda na kusisitiza kuwa ripoti hiyo imetolewa kwa malengo ya kisiasa.Ripoti ya wiki hii ya IAEA imedai kuwa Iran iko mbioni kuunda bomu la nyuklia lakini viongozi wa Tehran wamekanusha vikali tuhuma hizo zisizokuwa na msingi.